Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Mhe. Jaji Imani Aboud amependekezwa kugombea Urais wa Mahakama hiyo. Jaji Aboud amesema endapo atashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika…